Alhamisi 18 Septemba 2025 - 22:47
Damu ya Mashahidi ni Taa ya Njia ya Quds na Hazina ya Ushindi kwa Ummah wa Kiislamu

Hawza/ Seyyed Abdulmalik Badruddin Al-Houthi, kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, katika kujibu ujumbe wa rambirambi kutoka kwa Abul-Alaa Al-Wala’i, alieleza kuwa kupata shahad rais wa Serikali ya Mageuzi na Maendeleo ya Iraq pamoja na wafuasi wake ni fahari kwa Ummah ya Kiislamu, na alisisitiza umuhimu wa kuendelea na jihadi katika nyanja zote dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Seyyed Abdulmalik Badruddin Al-Houthi, katika barua rasmi aliyomuandikia Abul-Alaa Al-Wala’i, aliuheshimu ujumbe wa rambirambi aliopokea kufuatia shada ya rais wa Serikali ya Mageuzi na Maendeleo ya Iraq na wafuasi wake.

Katika barua hiyo, iliyochapishwa chini ya kichwa cha habari cha “Harakati ya Qur’ani – Kamati ya Mashahidi”, alieleza kwamba; kifo cha kiongozi huyo na wafuasi wake ni “fahari kwa Ummah wa Kiislamu”, na kuongeza kuwa: “Damu safi ya mashahidi ni mali muhimu kwa ushindi wa Ummah na hatua muhimu katika njia ya ushindi mkubwa, tunajivunia kwamba mashahidi waliopoteza maisha yao kwa ajili ya Quds na katika jihadi takatifu, wamepata heshima ya juu ya shahada.”

Kiongozi wa Ansarullah, akirejelea uhalifu unaofanywa na utawala wa Kzayuni dhidi ya Wapalestina, alisisitiza umuhimu wa kuendelea na jihadi katika nyanja zote za Ummah ya Kiislamu.

Alimalizia barua hiyo kwa kutoa pongezi kwa siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saww), na kuuombea Ummah ya Wapalestina, hasa watu wa Ghaza, ushindi na ufumbuzi wa changamoto zao.

Barua hii ilisainiwa tarehe 10 Rabi’ul-Awwal 1447 Hijria, inayolingana na 15 Septemba 2025 Mwaka wa Miladi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha